Daah! Patana na mtoto 'anayeunda' pesa.

magician
magician

Haya ni mazingaumbwe ama maajabu ya Firauni?

Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 19 mjini Lagos Nigeria, amejulikana sana kwa vioja anavyo fanya na kugeuza vitu mbali mbali kuwa pesa.

Babs Cardini alipenda sanaa ya kufumba watu macho tangu alipokuwa na miaka 5 lakini alianza kufanya hivi vioja alipokuwa na umri wa miaka 16.

Akizungumza na wanahabari, Babs alisema akiwa mdogo, alikuwa anatazama filamu za ''mchezo wa fumba macho'' kwenye televisheni na kuwa na ari ya kunoa makali yake ili pia anawiri katika uigizaji huo.

Zaidi ya hayo, chikukizi huyu alisema kuwa alichukua muda mfupi sana kumakinika katika mnchezo wa 'kufumba macho'  na anaaamini kuwa ana kipawa cha aina yake kwani watu wengi huchukua muda mrefu kumakinika kwenye sanaa hii.

''I’m gifted,it takes time to learn these things but I did it under two days. It also surprised me as it took some people two years to master," alisema.

Babs Cardini alisimulia safari yake na kusema kwamba, siku yake ya kwanza kuzuzua umati, alimwambia rafiki yake achukue karata moja kati ya zile walizokuwa nazo kisha Babs akamwambia mwenzake ni karata ipi aliokuwa amechukua bila hata kuona ni gani alikuwa amechagua.

Cardini ni muislamu na mara kwa mara amekashifikwa na waislamu wenzake lakini kijana huyu alishikilia kuwa hawezi acha sanaa hii na kwamba anazidi kumuomba Mola amsaidie anawiri zaidi ;katika mchezo wa kufumba macho.

"Mimi ni Muislamu na siku moja niliambiwa kuwa dini ya Kislamu haiungi mkono mambo kama haya kwa sababu yanakaa ya kishetani na anayefanya mambo hayo anastahili kuuawa. Pia mimi huswali.   Lakini sitegemei maombi pekee," alisema.

Licha ya hayo, kijana huyu alisema kuwa akiona vioja vya kumfurahisha kwenye runinga yeye huandika mahali na kusema kuwa atajaribu kuiga.

Amini usiamini, chipukizi huyu hufanya vioja vyake bila malipo kwani haitishi  mtu yeyote pesa kwasababu kwake yeye ni hali moja moja kufurahisha nafsi yake.

Changamoto kuu kwake ni kwamba mara nyingi watu wengi wanaokuja kuona ustadi wake huomba tu  abadilishe vitu kuwa pesa.

"akili ya watu wengi wanapoona mtu ni ''magician'' wao hutaka tu pesa," alisema.

Licha ya hayo, kijana huyu anajivunia talanta yake kwani watu wengi mjini Lagos huvutiwa sana na vioja vyake na hata wengi  kutaka  kuwa rafiki yake.

 BBC