logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Imepita miezi 7 tangu tulipoacha vileo ili kuzingatia maisha yetu na Mungu – Anerlisa Muigai afichua

“Kuna vitu vingine ambavyo haviwezi kosa kwa nyumba. Ribena,” Muigai aandika

image
na Achieng' Kezia

Dakia-udaku16 October 2024 - 16:34

Muhtasari


  • Anerlisa Muigai afichua kwamba yeye na mumewe waliwacha vileo ili kuzingatia maisha yao na Mungu
  • Imepita miezi 7 tangu walipoacha vileo


Mfanyibiashara Anerlisa Muigai atangaza imepita miezi saba tangu aache pombe yeye pamoja na mumewe.


Muigai alifichua habari hizo kwa chapisho kupitia Instagram ambapo aliandika kwamba yeye na mumewe waliwacha vileo ili kuzingatia maisha yao na Mungu.


“Kuna vitu vingine ambavyo haviwezi kosa kwa nyumba. Ribena. Mimi sio shabiki lakini mume wangu anazipenda sana. Tuliacha vileo ili kuzingatia maisha yetu na Mungu. Mimi, niligundua napenda maji na chai ya mitishamba. Inaelekea miezi 7 bila pombe pamoja na mume wangu,” Muigai aliandika.


Mapema mwezi Julai Muigai alitangaza kupata wokovu na kusema anafurahia maisha yake yaliyojaa amani.


“Nina furaha kumpa Kristo maisha yangu. Maisha yangu ina amani sana. Watu ambao nimewachagua katika maisha yangu ni kila kitu nilichotaka. Mungu ndiye njia pekee. Anakuja kwanza,”


Mwezi wa Machi Anerlisa alitangaza kuchumbiwa na mpenzi wake Melvin Ibrahim.


Uchumba wa Muigai unakuja baada ya talaka yake na mwimbaji wa Tanzania Ben Pol mnamo 2021, baada yao kuchumbiana mnamo 2020.


Kwa mahojiano Ben Pol alisema kuwa hakufurahia ndoa yake na Muigai.


“Kusema ukweli, sifai kuwa mwongo, sikufurahia sana ndoa. Ndoa ina mpango wa kupata watoto, sijawai ona. Sikuona ndoa kama wanavyoona na watu wengine,”


Mwimbaji huyo alisema kuwa uhusiano wake na Anerlisa ulikuwa wa kwanza wa kweli kutokea katika maisha yake na hivyo alikuwa na matumaini makubwa ya ndoa nzuri.


Alikiri kwamba alikuwa amewekezea hisia na mapenzi yake yote katika uhusiano huo kabla ya mambo kuharibika.


“Kiwango cha upendo, kiwango cha kujitolea ambacho nilikuwa nimempea hakikuwai tokea. Sijawai kumpenda mtu mwingine kabla yeye. Ilikuwa ni uhusiano wa kwanza ambayo nilizama na nilikuwa sawa,” alisema.


Ben aliweka wazi kwamba ndoa yao haikuvunjika kwa sababu ya masuala ya kukosa uaminifu.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved