logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Warren avunja kimya kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wake na Whitney

“Binafsi mimi nina uzoefu mbaya sana na marafiki kwa sababu marafiki sio watu wa kuamini,” Warren amesema

image
na Achieng' Kezia

Dakia-udaku17 October 2024 - 13:26

Muhtasari


  • Warren amefunguka kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wake na mpenzi na mama mtoto wake Whitney
  • Whitney alipata ujauzito akiwa katika mwaka wake wa kwanza wa chuo kikuu

Muundaji maudhui Warren ametangaza kuachana na mpenzi wake Whitney miezi chache baada ya wao kupata mtoto wao wa kwanza.


Kupitia video iliyochapishwa YouTube, Warren anasema kuwa yuko tayari kuondoka nyumbani na kumuachia Whitney nyumba yao kwa kuwa yeye anataka uhuru wake.


“Lakini siendi na chochote, namuachia kila kitu. Hii nyumba yote ni yake niataka tu uhuru wangu,”


Warren anasema kuwa aliona tabia za mpenzi wake zikiwa tofauti, kitu ambacho kilimfanya kuchukua simu yake na kuangalia aliyekuwa akizungumza naye.


Alipata kuwa Whitney alikuwa akimwambia rafiki yake shida zake, jambo ambalo halikumfurahisha kwa sababu haamini marafiki



“Binafsi mimi nina uzoefu mbaya sana na marafiki kwa sababu marafiki sio watu wa kuamini,”



Aliendelea na kusema kwamba alikuwa tayari kukaa kwa uhusiano lakini heshima haipo tena.



“Mimi nilikuwa tayari kukaa lakini msichana wenyu hanitaki. Alianza kunionyesha madharau, disrespect inaongezeka hapa na pale. Heshima haipo tena,” alisema


Warren alisema heri atafute chokoraa ampende kuliko kukaa na tajiri ambaye hampendi.


“Mimi nimetoka huko Kisii hata kama mimi ni chokoraa wacha nitafute chokoraa mwenzangu basi anipende kuliko kukaa na tajiri mwenye hanipendi,”


Pia alisema kuwa atamfanyia mwanawe chochote kwa sababu anampenda sana na kuwa hataki kufanya chochote ambacho kitamuathiri hapo mbeleni.


“Mimi yule mtoto nampenda na roho yangu yote. Nitafanya kitu chochote kwa hii dunia huyo mtoto aishi maisha fiti,”


Mashabiki walipoomuliza mahali Whitney yupo alisema kuwa yuko kwa nyumba ila hawaongeleshani.


“Ako hapa kwa nyumba nobody is talking to anybody,”


Warren alisema kuwa amevunjika moyo na anahitaji muda kufikiria kila kitu ambacho kimekuwa kikitokea.


“Mimi nimevunjika moyo vibaya sana na kwa hiyo sababu nataka kwanza nichukue muda nifikirie kuhusu kila kitu ambacho kimekuwa kikifanyika,”


Whitney alitangaza kuwa mjamzito akiwa  mwaka wake wa kwanza katika chuo kikuu na umri wa miaka 19 kisa ambacho hakikupendeza watu wengi.


Warren na Whitney walijaliwa mtoto wa kiume miezi chache zimepita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved