logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nataka kuzeeka pamoja nawe!” Diana amhakikishia Bahati huku wakisherehekea miaka 8 ya mahusiano yao

Bahati lidokeza kuhusu kutaka kumpa Diana zawadi nane tofauti ili kuashiria hatua hiyo muhimu.

image
na SAMUEL MAINAjournalist

Dakia-udaku21 October 2024 - 09:52

Muhtasari


  • Jumapili wapenzi maarufu wa Kenya Kelvin Bahati na mwanavlogu Diana Marua waliadhimisha miaka minane ya uhusiano wao. 
  •  Diana Marua alikumbuka jinsi mumewe alimpa zawadi kadhaa kubwa na kumlipia mahari mwaka mmoja uliopita

Siku ya Jumapili, Oktoba 20, wapenzi maarufu wa Kenya mwimbaji Kelvin Bahati na mwanavlogu Diana Marua waliadhimisha miaka minane ya uhusiano wao. 

Wawili hao ambao wana watoto watatu pamoja walitumia siku hiyo kusherehekeana na pia kusherehekea safari yao ya mapenzi.

Katika ujumbe wake, Diana Marua alikumbuka jinsi mumewe alimpa zawadi kadhaa kubwa na kumlipia mahari mwaka mmoja uliopita.

"Leo, ukweli kwamba ni mwaka mwingine na wewe, ni Zawadi kubwa zaidi ambayo ningeweza kuuliza. Umeyafanya maisha yangu kuwa Mazuri sana, unanimwagilia maji kila siku, ninachanua kama ua bustanini. Umenipenda milele, na umefanya maisha kuwa ya thamani. Kila siku karibu na wewe ni Baraka ambayo siichukulii kirahisi,” Diana aliandika kwenye Instagram.

Mwanablogu huyo wa YouTube aliendelea kumhakikishia mumewe kuhusu jinsi anavyompenda sana na kumhakikishia kuwa anamtosha.

“Ndoto zetu ni Kubwa kuliko za jana na siwezi kusubiri kuuonyesha ulimwengu kile kinachotungoja mbeleni. Nina Wasiwasi na Nina Furahia Kinachokuja kesho. Tufanye hivi Babe, Tuishi maisha na kuyaishi kwa Utimilifu wake. ASANTE KWA YOTE,” alisema.

Diana pia alimtakia mumewe kumbukumbu njema ya mahusiano yao na akamwomba Mungu awaweke hai kwa ajili ya kila mmoja wao.

Bahati kwa upande wake alikuwa na ujumbe mfupi kwa mkewe Diana Marua ambapo alimtakia kumbukumbu njemaya mahusiano yao tu.

Pia alidokeza kuhusu kutaka kumpa mama huyo watoto wake watatu zawadi nane tofauti ili kuashiria hatua hiyo muhimu.

Je, uko tayari kwa zawadi nane za kusherehekea hii ama niwache tu. Kheri ya kumbukumbu ya mahusiano mpenzi wangu,” Bahati alimwambia mkewe.

Katika majibu yake, Diana alimwambia, "Nataka tu kuzeeka na wewe, unatosha."

Wapenzi hao wawili walianza kuchumbiana mwaka wa 2016 na tangu wakati huo wamejaliwa watoto watatu pamoja.

 

Katika majibu yake, Diana alimwambia, "Nataka tu kuzeeka na wewe, unatosha."

 

Wapenzi hao wawili walianza kuchumbiana mwaka wa 2016 na tangu wakati huo wamejaliwa watoto watatu pamoja.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved