Daktari kufika mahakamani akitaka ukeketaji wa wasichana kuhalalishwa.

Kiongozi wa jamii ya Maasai ambaye pia ni daktari atatoa ushahidi katika kesi inayotaka kubadilishwa kwa  sheria dhidi ya ukeketaji wa wasichana.

Daktari Tatu Kamau anasema kuwa wanawake wote haswa wale waliotimu umri wa miaka 18, wanapaswa kukubaliwa kufanya uamuzi kuhusiana na mili yao bila ya kuzuiwa na sheria.

Kamau anataka bodi ya kupambana na ukeketwaji wa wanawake ambayo imekuwa ikikabiliana na  mila hiyo kuvunjiliwa  mbali.

Jopo hilo la  majaji watatu linalowajumuisha  jaji Lydia Achode, George Kimondo na Margaret Muigai lnashughulikia kesi hiyo.

Kamau ambaye hatawakilishwa na wakali anasema jina "Kukeketwa" ni jina la kikoloni ambalo tulipewa na wale wasiolielewa.

Kamau aliwaambia majaji kwamba ukeketwaji wa wanawake ni sehemu ya mila na desturi za kiafrika za kale kabla ya ukoloni na haufai jambo la hatia.

Aliendelea kuwaambia majaji hao kwamba atakuwa shahidi katika kesi hiyo na ataoneshana kanda ya video ili kujaribu kuwashawishi kukubaliana naye.

Afisa wa polisi wa zamani John Arap Koech ambaye alifika mbele ya mahakama kama amevalia mavazi ya kitamaduni pia anamuunga Kamau mkono.

Koech anasema pia yeye atatoa ushahidi wake ili kuieleza mahakama kwanini ukeketwaji wa wasichana unafaa kuhalalishwa.

“Mheshimiwa hii FGM tutafanya kwa makini tujue ubaya ni nini," aliiambia mahakama.

Hata hivyo mashirika ya kupigania haki za kibiandam yamepinga kuhalalalishwa kwa zoezi hilo.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 30 mwezi Julai.