Daktari Stella Bosire kukataa uteuzi wa gavana wa Nairobi Mike Sonko

Sekta ya afya ya kaunti ya Nairobi itabaki kuwa wazi kwa sababu Daktari Stella Bosire aliweza kukataa uteuzi wa gavana wa Nairobi Mike Sonko.

Borire ambaye alikuwa anapaswa kuenda mbele ya kamitii ya kata ndogo ya kaunti ya Nairobi kwa ajili ya uteuzi huo, alikosa kuonekana kwa ajili ya uteuzi Jumatatu.

Kaimu msemaji wa kata ndogo ya Nairobi Chege Mwaura alisema Bosire hajawahi peana vyeti vyake kama ilivyo madhumuni ya uteuzi.

"Tulidhani kuwa hakuwa na nia ya nafasi hiyo, kwa sababu hajawahi leta makaratasi au vyeti vyake katika kamitii." Alizungumza Chege.

Bosire alikuwa miongoni mwa wanawake watano ambao waliteuliwa na gavana wa kaunti ya Nairobi Januari kwa kujaza nafasi iliyokuwa wazi katika baraza la mawaziri.

Kwa upande wake Bosire alisema kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo yange hitaji kuzingatiwa kabla ya kukubali uteuzi huo wa gavana Mike Sonko.

Alinakili mtindo wa uongozi wa gavana huo kuwa unakwaruza, pia na kukosa heshima katika utaalamu, kukosa uadilifu na kadhalika.

Pia alitaka mambo kadhaa kuweza kusemwa kama vile uajibikaji na uwazi katika matumizi ya mali ya umma, dhamira ya kisiasa na upendeleo katika kaunti.

"Kwa bahati mbaya imefikia hicho kiwango, lakini nitaweza kuhudumia wananchi wa Kenya katika nafasi ingine." Alizungumza Bosire.

Kabla ya uteuzi huo Borire alikuwa anafanya kazi katika hospitali ya Kiambu kama mrakibu wa matibabu.

Hata hivyo gavana Mike Sonko alisema kuwa ataweza kuteuwa mtu mwingine ili aweze kufanya kazi katika sekta hiyo na kujaza nafasi hiyo ya daktari Stella Bosire ambayo aliweza kuikataa.

"Bosire aliweza kuletwa kwangu na mtu ambaye ninamuamini, kwa sababu nilitakamwanamke ambaye ana elimu ya kiafya,

"Hata hivyo nitamteua mtu mwingine, hizi vitu ni za kawaida na uwa zinatendeka." Alizungumza Sonko.

Mtendaji wa ardhi Charles Kerich amekuwa katika sekta hiyo tangu mwaka jana Septemba wakati Sonko alipomsimamisha kazi Vesca Kagongo ambaye pia alikua kaimu katika sekta hiyo.