Doreen Adisa Lugaliki, 38, alikuwa tayari keshatakiwa wafunge ndoa na mpenzi wake Fred Mboss mwenye umri wa miaka 45 .wawili hao walikutana mwaka wa 2017
“ Nilimpenda kwa sababu ya urembo wake ,tabia na werevu wake .wazazi wetu walikuwa na furaha sana tulipowamabia kuhusu mipango yetu na waliahidi kutuunga mkono’ Mboss ameliambia gazeti la The Star kwa njia ya simu .
Wawili hao walikuwa wakiingoja serikali iruhusu usafiri wa kuingia na kutoka Nairobi ili kuwtembelea wazazi wa Adisa huko Bungoma
“ Ziara hiyo ingefuatiwa na mazungumzo kuhusu mahari kabla ya harusi ,mipango ya harusi ilikuwa ikiendelea’ amesema Mboss .
Mipango hiyo hata hivyo ilitumbukia nyingo wakati Adisa alipoanza kuugua julai tarehe 5 na Mboss akambikimbiza katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan . alipatikana na ugonjwa wa kisukari na kulazwa saa nne usiku .
Hali yake ilianza kuwa mbaya julai tarehe 7 baada ya kupimwa na kupatikana na virusi vya corona kisha baadaye aakahamishwa hadi kitengo cha ICU .
“ Aliaga dunia kwa sababu ya matatizo yanayotokana na COVID 19 julai tarehe 10’ familia yake iliwaarifu waombolezaji Bungoma wakati wa maazishi yake . Madaktari waaliweza kugundua kwamba Adisa aliupata ugonjwa huo kutoka kwa mwenzake ambaye aliambukizwa na mgonjwa katika Nairobi South Hospital ambako alikuwa akifanya kazi l kama mwanajinakolojia . Mboss alisema atakosa sana safari zao walizofanya kwenda Singapore ,Dubai na sehemu nyingine za dunia . “ Ntaikosa sana tabasamu yako nzuri na akli zangu pevu’ amesema
Adisa awali alikuwa ameolewa na Kituku Kinyae mwaka wa 2007. Haijabainika iwapo walitalakiana kwa njia rasmi .Aliwacha watoto wake pacha Kyla Ndinda na Kyle Kimilu .