Mfanyikazi wa KQ Ali Gire ambaye amesimamishwa kazi kwa kupiga picha ya video na kuisambaza ndege ya China Southern Airlines ikitua katika uwanja wa JKIA ikiwa na abiria 239 siku ya jumatano sasa amesema maisha yake yamo hatarini .
Wakati ikitangaza kumsimamisha kazi KQ ilimshtumu kwa kukiuka sera za kampuni kutokana na jinsi alivyoshughulikia tuki hilo baada ya video yake kuonyesha raia wa China wakiwasili nchini licha ya hofu ya uwezekano wa kuleta virusi vya Corona Kenya .
Video hiyo iliwafanya wakenya kuhamakishwa na hatua ya serikali kulichukulia suala hilo kwa wepesi huku matifa mengi duniani yakipiga marufuku safari za ndege kuingia nchini mwazo ili kuzuia usambaaji wa virusi hivyo. Siku ya ijumaa ,Ali alithibitisha kwamba amesimamishwa kazi huku wengi mtandaoni wakimtetea na kulaani hatua ya KQ kumfurusha kazini .