Wanandoa hao wametangaza hilo wiki sita tu baada ya kurejea kutoka safarini Canada walipokuwa katika mapumziko na hatua ya kujiondoa kutoka majukumu ya kifalme imeonekana kama jambo kubwa na ambalo hakuna aliyewahi kufikiria linaweza kutokea . Wandani wanaotetea kuwepo kwa familia ya kifalme na mfumo wake wa maisha wameshangaa mbona Harry na Meghan waliopewa kila kitu ,Harusi waliotaka,nyumba waliotaka ,pesa na safari za nje ya Uingereza walivyoamua ghafla bila kumshauri yeyote kuondoka familia ya kifalme .
Harry na Meghan hata hivyo wamesema wako tayari kuendelea kumsaidia Malkia katika majukumu yake ya kifalme na pia kuanza mkondo mpya wa maisha yao ili kupata uhuru wa kifedha na kumlea mwanao katika mazingira ya ukuuzi wa kifalme . Katika taarifa iliyotolewa na Kasri ya Buckingham imesema - ‘Mazungumzo kati ya Duke na Duchess wa Sussex yapo katika hatua za mwanzo . tunaeleewa ari yao ya kutaka kuchukua mkondo tofauti ,lakini masuala haya ni mazito na itachukuamuda kuyajadili’.‘Usiri mkubwa uliozingira uamuzi wa wawili hao ni kama kisu kilichowachoma kabisa watu wote wa familia ya kifalme.Ni kama usaliti mkubwa sana’ mndano mmoja wa Kasri amenukuliwa akisema .