David Ouma ataja kikosi cha Harambee starlets

Koach wa Harambee starlets,David Ouma amekitaja kikosi cha wachezaji 39 watakaoiwakilisha Kenya kwenye mechi za kuwania tiketi ya kufuzu katika mashindano ya Olimpics nChini Japana mwaka 2020.

Kenya inatarajiwa kucheza na Malawi huku wakikabana koo na Ghana ama Gabon iwapo watawagaragaza Malawi. Asilimia kubwa ya wachezaji waliotajwa waliwakilisha Harambee starlets kwenye mechi za kufuzu na kucheza AFCON upande wa wanawake katika mechi za Uganda na Equatorial Guinea mwaka uliopita.

Wachezaji hao wanatarajiwa kufika kambini Camp Toyoyo tarehe 14  mwezi julai hapa mjini Nairobi. Hatahivyo, wakali hao wanatarajiwa kuruhusiwa kujiunga na timu zao wikendi ili kuyatumikia majukumu ya ligi ya vilabu vyao.

Mechi ya mkondo wa kwanza inatarajiwa kuchezwa tarehe 28 mwezi wa nane huku mechi ya marudiano ikichezwa tarehe 1 mwezi septemba. Michuano hiyo ya mwaka 2020 itakuwa awamu ya 5  ya Olympics itakayoandaliwa nchini Japan.

Kikosi kilichotajwa:

WALINDA LANGOhttps://radiojambo.co.ke/hassan-oktay-ajiweka-mbali-na-madai-yake-manishinmwe/

Wilfrida Seda (Vihiga Queens), Judith Osimbo (Gaspo Youth), Elizabeth Atieno (Wadadia), Annette Kundu (Eldoret Falcons), Lilian Awuor (Vihiga Queens)

WALINZI

Lilian Adera (Vihiga Queens), Maureen Khakasa (Trans Nzoia Falcons), Vivian Nasaka (Vihiga Queens), Enez Mango (Vihiga Queens), Dorcas Sikobe (Oserian), Esther Nadika (Gaspo), Lucy Akoth (Mathare United Women), Lidiah Nasike (Makolanders), Lydia Akoth (Thika Queens), Stella Anyango (Gaspo)

VIUNGO

Myline Awuor (Vihiga Queens), Sheril Angachi (Gaspo), Cynthia Shilwatso (Vihiga Queens), Vivian Corazone (Gaspo), Yvonne Kavere (Soccer Queens), Cynthia Matekwa (Nyuki Starlets), Janet Bundi (Eldoret Falcons), Rebecca Akinyi (Oserian Ladies), Maurine Achieng (Vihiga Queens), Martha Amunyolete (Trans Nzoia Falcons), Bertha Omita (Kisumu All Starlets), Mwanahalima Adam (Thika Queens), Rachael Muema (Thika Queens), Elizabeth Wambui (Thika Queens)

WASHAMBULIZI

Topista Nafula (Vihiga Queens), Tumaini Waliaula (Trans Nzoia Falcons), Mercy Airo (Kisumu All Starlets), Phoebe Owiti (Vihiga Queens), Terry Engesha (Vihiga Queens), Susan Muhonja (Trans Nzoia Falcons), Cynthia Achieng (Kisumu All Starlets), Winnie Kanyotu (Gaspo Youth), Elizabeth Katungwa (Kwale Girls)

.