David Rudisha aruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kutibiwa kufuatia ajali

Bingwa wa dunia wa riadha David Rudisha alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani jana baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani huko Nyamira. Gari ya Rudisha iligongana ana kwa ana na basi lililokuwa likielekea Nairobi kutoka Kisii.

OCPD wa Keroka Walter Opondo anasema Rudisha hata hivyo alinususrika na majeraha madogo.

Bingwa huyo alikimbizwa katika hospitali mjini Nairobi siku ya Jumapili, kwa matibabu zaidi baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani eneo la Kijauri, Borabu, Kaunti ya Nyamira.

Kakake Shadrick Rudisha aliambia The Star kupitia simu kwamba, walikuwa njiani kuja Nairobi ili afanyiwe uchunguzi zaidi kubaini kama alipata majeraha yoyote ya ndani wakati gari lake lilipogongana ana kwa ana na basi la Ena Coach lililokuwa likielekea Nairobi kutoka Kisii.

“We are going for secondary checks to affirm if he sustained any further injuries to his body,” Shadrick alisema.

“Gari la mwanariadha huyo liliharibika vibaya sehemu ya mbele,” OCPD wa Keroka Walter Opondo alisema.

Bado haijabainika kama ni Rudisha mwenyewe aliyekuwa akiendesha gari hilo wakati wa ajali.

Rudisha alikuwa anaelekea nyumbani kwao kutoka Nairobi, Shadrick alisema.