Kinoti analalamika kwamba madai yanayoibuliwa na Wairimu ni njama za kutumia mamlaka vibaya huku wakili huyo akitumia fursa hiyo kulipiza kisasi ambaye imekuwa ikidumu baina ya mkuu wa mwendesha mashtaka na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai.
''Mahakama inafaa kufahamishwa kisheria kwamba Sarah Wairimu na wakili wake Phillip Murgor wamekuwa kabla, na baada ya kukamatwa, katika kila chombo cha habari ikiwemo Youtube wakisimulia na kupeana mtazamo mbadala wa matukio kuhusu kesi hii, na iwapo kuna yeyeyote anayekiuka amri ya kortini ni hao wawili," alisema.
Aliendelea kudai kwamba mshukiwa anatumia kuendeleza juhudi zake za kujitetea katika kesi inayomkabili kuhusu kifo cha mumewe.
Akijibu madai hayo ya Wairimu, Kinoti anasema kwamba hiyo ni mikakati yake (Wairimu) inayopangwa ya kujaribu kujitetea dhidi ya mashtaka.
Kinoti aliendelea kusema kwamba madai hayo yanakusudiwa na ni mikakati ya mshtakiwa na wakili wake kujitetea mapema kabla ya kesi yake kusikilizwa tena..
Isitoshe anasema kwamba korti haijatoa amri ya siku 30 kama jinsi inavyotakikana kabla ya kuzua madai mapya, aliongeza kusema kuwa Sarah alikuwa akiibua masuala ya urithi wa mali nje ya korti.
Kinoti anadai kwamba Wairimu na Murgor wanataka kutawala uchunguzi na mashataka ya kesi kama DPP na DCI huku sawia wakijitetea kama washtakiwa.