DCI kusukuma mashtaka dhidi ya Henry Rotich

1777725
1777725
Ni siku ya pili tangu waziri wa hazina Henry Rotich kuenda katika ofisi ya DCI ili kuijibu maswali kuhusiana na kashfa za mabwawa, waziri huyo aliweza kufika katika ofisi hiyo iliyoko katika barabara ya Kiambu saa tatu kamili.

Ilhali wakili wake Katwa Kigen aliweza kufika mapema.

Usiku wa jana Rotich aliweza kutoka ofisini mwa DCI dakika chache baada ya saa tatu usiku, wachunguzi wa karibu sana waliweza kuambia vyombo vya habari kuwa polisi waliweza kupata sababu za mashtaka dhidi ya waziri huyo baada ya kujibu maswali kwa mara ya tatu.

"Tunge pendekeza mashtaka yake kwa kushindwa kulinda fedha za serikali na umma," Alisema mkuu wa polisi asiyetaka kujulikana.

Vyombo vya habari jana viliweza weka imara kuwa wachunguzi walikuwa wametilia mkazo kwa bilioni 21 zilizotolewa na hazina hiyo kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa hayo mawili.

"Tunataka kujua usalama wa fedha za umma, licha ya kampuni ulioipa pesa za ujenzi wa mabwawa kwa sasa imekumbwa na tatizo la fedha." Aliuliza mmoja wa wachunguzi.

Wiki ijayo wachunguzi wa DCI wataweza kuwaita maafisa wakuu wa kutoka kwa wizara ya kilimo kuwauliza maswali kuhusiano na mabwawa hayo.

Jumanne Rotich aliweza kujibu maswali ya wachunguzi kwa muda wa masaa 13.

Wanahabari wa DCI walisema kuwa Rotich pia alitarajiwa kupeana maelezo zaidi kuhusu mabwawa hayo mawili, maafisa kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP) ambao wanasaidia katika uchunguzi huo, waliweza kutoa masuala ambayo wachunguzi wangepaswa kumuuliza waziri.

Katibu wa kudumu wa hazina Kamau Thugge, ambaye ni afisa wa uhasibu katika wizara hiyo aliweza kurekodi kauli na polisi kuhusiana na uchunguzi unao endelea.

Rotich, wiki jana alisema kuwa malipo hayo ya mapema ya ujenzi wa mabwawa yaliweza kufanyika chini ya sheria.