Dennis Odhiambo kuwa nahodha wa Harambee Stars dhidi ya Tanzania

dennis odhiambo
dennis odhiambo
Kiungo wa kati wa sofapaka  Dennis Odhiambo atakuwa nahodha wa kikosi cha harambee stars watakapokutana na Tanzania ugenini katika mchuano wa mkondo wa kwanza wa mechi ya kufuzu kwa kombe la CHAN.

Cliffton miheso aliyekosa majukumu ya timu ya taifa katika mechi za kombe la afcon ameitwa katika kikosi hicho cha wachezaji 22 kilichotajwa na kocha Sebastien Migne.

Mlinzi wa kilabu ya Mathare United Johnstone Omurwa, aliyeitwa katika timu ya taifa katikati ya wiki pia ame orodheshwa katika timu hiyo  pamoja na mchezaji wa timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Musa Masika.

Tukivuka boda,

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameiweka bayana kwa naibu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward kwamba anataka kumsajili Harry Maguire haraka iwezekanavyo. Leicester hawataki kumwachilia Maguire kwa chini ya pauni milioni 80, ambayo ni pauni milioni 10 zaidi ya ofa ya United.

Maguire anaaminika kutaka kusalia Leicester lakini angependa kuhamia Old Trafford iwapo klabu hizo mbili zitakubaliana mkataba. Manchester City pia wameonyesha nia ya kumtaka Maguire.

Mcheezaji  wa kilabu ya  Leicester Demarai Gray amesema hakuna kinachofaa kuzua wasi wasi kuhusiana na uhamisho ulioripotiwa wa Harry Maguire na haamini kwamba mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 26 amenuna kwa ajili ya kutokupigwa hatua yoyote kuhusiana na na uhamisho wake.

Maneja wa Liverpool Jurgen Klopp amepuuza ripoti kwamba kilabu hiyo inalenga kumsajili mshambuliaji wa real Madrid na Wales Gareth Bale mwenye umri wa miaka 30. Ameshikilia kwamba wajibu wake sasa ni kukiboresha kikosi chake na sio kuwanuanua wachezaji wapya.

Manchester United wameomba kufahamishwa kuhusu hatma ya mchezaji Christian Eriksen mwenye umri wa miaka 27 wa Tottenham. Kandarasi ya nyota huyo wa kimataifa wa Denmark imesalia na mwaka mmoja kukamilika na huenda akauzwa kwa pauni milioni 70.

United pia inamlenga mshambuliaji wa Lille na nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Nicolas Pepe mwenye umri wa miaka 24, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 70, kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku endapo atajiunga na Inter Milan.