Mshambulizi huyo pia amefichua kwamba atapumzika soka hadi Disemba, akiendela kufuatilia kesi dhidi ya klabu yake ya zamani. Anasema klabu hio haikumpa fursa ya kujitetea.
Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier amekanusha madai kua klabu hio ilitoa hundi bandia kwa John Mark Makwatta katika juhudi za kumsajili mshambulizi huo.
Rachier anadai ni Makwatta aliyetaka kujiunga na Gor baada ya kutembela ofisi za klabu hio Jumatatu, na ripoti kua mshambulizi huyo wa zamani wa Ulinzi Stars alipewa hundi bandia si za ukweli.
Rachier pia amefichua kwamba Makwatta ameomba radhi kuhusiana na madai hayo. Makwatta kisha alijiunga na mahasimu wa Gor Mahia, AFC Leopards.
Hayo yakijiri, Michael Olunga amewasili nchini kujiunga na kikosi cha Harambee Stars ambacho kiko kambini kabla ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya Uganda.
Francis Kimanzi anamtarajia Ayub Timbe anayesakata soka Uchina anayetarajiwa kuwasili hii leo ili kukamilisha kikosi chake. Huku ikiwa Bernard Ochieng ana jeraha na Joseph Okumu badi akiwa anakita miziz Uswidi baada ya kujiunga na IF Elfsborg mwezi uliopita, Kimanzi amemwita Brian Otieno wa Bandari na Johnstone Omurwa wa Wazito kuchukua nafasi zao.
Mechi hio itachezwa Jumapili hii uwanjani Kasarani.