Dennis Oliech bado anauguza jeraha la msimu uliopita - Rachier

Kiungo wa Gor Mahia Dennis Oliech bado anapona jeraha alilolipata msimu uliopita na hajawasili kwa mazoezi, mwenyekiti Ambrose Rachier amethibitisha.

Oliech alijeruhiwa mwishoni mwa msimu uliopita na anatarajiwa kukosa mwanzo wa msimu mpya utakaoanza tarehe 30 mwezi huu. Kukosekana kwake ni pigo kubwa kwa klabu hio ambayo tayari imempoteza Jacques Tuyisenge.

Kundi la pili la timu ya kinadada ya voliboli liliondoka nchini jana usiku kuelekea Italia kwa michuano ya kufuzu kwa Olimpiki ya mabara. Timu hiyo inajumuisha Trizah Atuka, Jane Wacu, Laureen Ekaru na pia msaidizi wa kocha Josphat Barasa.

Kundi la kwanza lilisafiri jumanne. Michuano hiyo itaanza hapo kesho huku Kenya ikikabana na Ubelgiji, Uholanzi na Uruguay. KVF inapanga kutumia kipute hicho kuwatayarisha kinadada hao kwa michuano ya Africa baadae mwezi January. Kenya ilishiriki Olimpiki mara ya mwisho mwaka wa 2004.

Mchezaji wa Simbas Isaac Njoroge hatacheza katika kipute cha Victoria Cup dhidi ya  Zimbabwe kwa kuwa na jereha la kichwa. Mchezaji huyo wa KCB alipata jeraha hilo waliwapowanyuka Zambia huko Kitwe wikendi iliyopita.

Njoroge amekua na wakati mzuri na Simbas, akianza katika mechi waliyofunga Uganda mjini Kampala na kusaidia katika ushindi wao dhidi ya Zambia. Kocha Paul Odera anatarajia Njoroge atapona kabisa na kuwa tayari kucheza dhidi ya Zambia katika mchuano wa marudio mwezi ujao.