Dereva wa Trela afariki katika ajali kwenye barabara ya Eldoret-Malaba

Dereva mmoja wa trela ameaga dunia mapema leo katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea katika eneo la Ndengelwa kwenye Barbara kuu ya Eldoret- Malaba.

Kulingana na walioshuhudia ajali hio iliyohusisha treila tatu, treila moja ilikua ikitoka Tororo kuelekea Eldoret na ilijaribu kukwepa treila nyingine ambayo ilikua imeegeshwa barabarani, baada ya kukumbwa na hitilafu, kabla ya kugongana ana kwa ana na treila nyingine iliyokua ikitoka Eldoret kuelekea Malaba ikiwa imebeba bidhaa za kutengeza simiti.

Dereva wa treila hiyo aliyejulikana Kama Katana alifariki papo hapo.

Mwili wake umepelekwa katika hifadhi maiti ya hospitali ya rufaa ya Bungoma.

Ajali hio imetokea siku chache tu baada ya watu nane kuaga dunia katika ajali nyingine katika eneo la Matulo kwenye barabara hio.