Diamond akana madai ya kuwatenga watoto wake

Diamond platinumz ameyajibu madai ya aliyekuwa mkewe Zari Hassan alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari vya Tanzania.

Hivi majuzi, Zari alisema kuwa Diamond amemuachia majukumu ya kuwalea watoto wao wote wawili huku ikisemekana kuwa Diamond hajawahi watembelea watoto wao kwa muda wa miezi tisa iliyopita.

Jambo hilo lilitokea baada ya Diamond kupiga picha watoto wake wawili kupitia njia ya 'screenshot' alipokuwa anazungumza nao kupitia njia ya video.

"Hata hakuzungumza nao. Alipiga simu kisha walipochukua akapiga picha na kukata simu kabla hawajaanza mazungumzo." Zari alisema.

Diamond amekanusha madai hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kule nchini Tanzania,"Suala la malezi ya watoto halinishangazi mimi kwa sasa. Wazazi wanapopeana talaka mambo mengi huzuka na hasa ya watoto ila natumai kuwa kila kitu kitakuwa sawa hivi karibuni."

"Juzi nilikuwa katika sherehe za siku ya kuzaliwa na mjomba wa watoto wangu na zari alinipigia simu. Nilikuwa na mtoto wangu na Hamisa Mobetto na tulizungumza naye." Diamond alisema.

Diamond aliongeza kuwa anaweza zungumza kuhusu wanawe ila sio kumhusu aliyekuwa mpenziwe Zari Hassan aliye na uhusiano kwa sasa.