Diamond akiri kumfuatilia Zari na mpenziwe katika mitandao ya kijamii

zari
zari
Diamond Platnumz akiri kuwa bado huwa anamjulia hali mke wake wa kitambo na mama ya watoto wake, Zari Hassan.

Hivyo ndiyo Diamond alipata kujua kuwa Zari alikuwa amesonga mbele na maisha yake na alikuwa anamuona kimapenzi 'King Bae'

''nina furaha kuwa ako kwenye uhusiano mwingine,'' Diamond alisema kwenye mahojiano na Wasafi FM.

Star huyu wa bongo alikiri kuwa hana hisia mbaya baada ya wanawe wawili - Tiffah na Nillan kukutana na King Bae.

"huwa naona video na picha akimleta mpenziwe ashinde usiku kucha. Naona pia video mpenziwe na wana wangu wawili  (wakikutana na wakihusishana)," Diamond alisema, kwangu hiyo ni furaha ya kweli kwa sababu Zari ana furaha.

Aliendelea kwa kusema, ''kitu ambacho kina maana kwangu ni ana mpenzi ambaye atakuwa mjomba mzuri kwa watoto wangu.''

Hata hivyo Diamond anaonekana kunywa mvinyo huku akihubiri maji.

Aliwacha kuwafuata watoto wake wawili.

Diamond aliweka wazi kuwa alitegemea Zari asonge mbele na maisha yake.

''mkiachana na mtu haimanishi kuwa wanafaa kubaki bila mahusiano. Niko sawa (na Zari kusonga mbele). La sina shida na hilo. Mwisho wa siku mkiachana wakona uhuru wa kusonga mbele."

Aliwashawishi mashabiki wake kuwa " nina furaha Zari amesonga mbele sanasana kwa sababu ikiwa hajasonga angetumia wakati wake kunichukia.''

Aliendelea kwa kusema kuwa yuko na furaha na uhusiano wake na mpenzi wake wa Kenya, Tanasha.