‘Diamond alinipenda hivyo’ Wema Sepetu afichua mbona alinyoa nywele zote kichwani

Wema Sepetu  ametambulika kwa jinsi alivyobadilisha muonekano wake mara nyingi, lakini hakuna aliyemtaraji kunyoa nywele zote na kusalia na  kichwa  kisafi miaka kadhaa iliyopita.

Wengi walishangaa ni kipi kilichomfanyikia ili kulazimu  hatua kama hiyo. Hata palizagaa uvumi kwamba alishauriwa kunyoa nywele zote baada ya kumzuru mganga  ili kumsaidia  arudiane na Diamond

Kama kioja kweli, walirudiana  baadaye  na wakasahau tofauti zilizoibuka kati yao. Lakini Wema sasa amepasua mbarika kuhusu kilichomfanya kunyoa hivyo kwani anasema alipata uhuru wa kuweza kuosha  kichwa chake alivyotaka.

Kupitia ukurasa wake wa instagram  muigizaji huyo alisema;

ThrowBack Thursday…

#NiMwendoWaViparaaaaa 

Ila kama ni kuthubutu jamani nilijuaga kuthubutu kwa kweli… Para Para kama ngozi… Afu nilikuwa naingia anywhere, anytime, anyhow… Nikioga naskia rahaaaa…  Afu wakati huo aliekua mpenzi wangu akawa anakihusudu kipara pia basi mambo yakawa BullBull… Maisha haya…. 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO