Tanasha 1

‘Diamond anavyomsukuma Zuchu sio kawaida.’ Adai meneja Jamal

Meneja wa msanii na mtangazaji Tanasha Donna,Jama Gadaffi akiwa kwenye mahojiano alidai kuwa msanii wa bongo Diamon anatumia nguvu nyingi kwa msanii Zuchu ili kumhujumu Tanasha ambaye ni mama wa mtoto wake.

Soma walichokuwa wanataka kufanya Tanasha Donna na Kevin Omwenga kabla ya kifo chake

Pia Jamal alidai kuwa ni jambo ambalo anahisi si njema na la kufanya.

Tanasha Donna
Tanasha Donna

“Mondi anatumia nguvu nyingi sana kwa Zuchu, ili amfunike mzazi mwenziwe…unaona live tu Diamond anavyo msukuma Zuchu sio kawaida tu ni sababu tu ya Tanasha, kutaka kuwalingnisha hao wawili. Lakini mimi naona kibiashara ni sawa, lakini mwishoni mwa siku  ni mzazi mwenzake, asingempa wakati mgumu.” Alisema Jamal.

Jamal alisema kuwa anapenda kazi ya msanii Zuchu lakini mtindo wake wa muziki ameutoa na kuiga kwa Tanasha.

“Kwanza mimi Zuchu namkubali sana, yuko vizuri Zuchu, napenda Kazi yake, ila kitu ambacho nilipost jana ni kwamba, Kuna nyimbo ya Tanasha ambayo iliweza kuvuja ambayo inaitwa ride, amemshirikisha Khaligraph Jones. So kuna miondoko flani hivi kaitumia Zuchu mimi nikahisi mbona kamuiga mwenzake.

Upendo wa baby mama: Hamisa Mobetto amposti Tanasha Donna na mwanawe

Katika Wasafi watu ambao niko karibu naona ni kama Romy Jons, Richardo Momo. Na hata kumcheki mtu kama Richardo Momo si hoja, lakini mimi nimeacha tu ipotelee kwenye mitandao, because it’s not that big. Mimi ni style tu mimi nilikuwa naongelea. Style flani hivi Tee anatumianga. So hiyo ati ni kitu kikubwa ati tutapigia hadi management.” Jamal Alizungumza.

Pia alidai kuwa Tanasha hajawahi lalamika kwa jambo lolote kuhusu Diamond,

Tanasha
Tanasha

“Hajawahi kulalamika hata siku moja, lakini ni vitu mimi naona sio lazima hata kuambiwa, jinsi kunavyo kwenda, sio lazima eti yeye aniambie kuko hivi.”

Photo Credits: radiojambo

Read More:

Comments

comments