Diamond Platinumz aahidi kuzilipia kodi familia 500 kwa miezi 3

Staa wa muziki nchini Tanzania Diamond ameahidi kuzilipia familia 500 kodi ya nyumba kwa miezi mitatu ijayo.

Diamond amefichua mpango huo wake katika instagram  akisema uamuzi wake umetokana na hali ngumu ambayo familia nyingi zinapitia kwa ajili ya janga la virusi vya Corona .

“ Ingawaje mimi ni miongoni mwa walioathiriwa na janga hilo, nitatumia kidogo nilichonacho kuwasaidia  watu wa familia 500 kulipa kodi zao." Diamond amesema

Diamond ameahidi kuanzisha mpango huo na atazitaja familia ambazo zitapokea msaada huo  siku ya Jumatatu Aprili tarehe 27