Diamond Platinumz asherehekea siku ya kuzaliwa ya bintiye

Bintiye Diamond Platinumz na aliyekuwa mpenziwe Zari Hassan, Princess Latiffah alifikisha umri wa miaka minne hio jana. Hivi juzi, Zari alisema kuwa Diamond hajawatembelea wanawawe kwa zaidi ya miezi tisa sasa huku pia akiyaacha majukumu yake kwa wanawe.

Diamond alimtakia bintiye siku njema ya kuzaliwa kwenye mtandao wake wa Instagrama kwa kumposti picha yake ikiwa na maelezo ya,"Daddy Loves You."

Kando na Diamond, mamaye mzazi pia alisherehekea siku ya kuzaliwa kwa mjukuu wake kwa ujumbe mfupi uliosema,"Happy Birthday mtoto Tiffah, roho yangu mimi kipenzi cha mama Dangote. Your grandma wishes you a long life full of blessings.I Love you."

Diamond na mamaye Latiffah, Zari walivunja uhusiano wao na kwa sasa Mr Platinumz anatoka na Tanasha Donna kimapenzi na wawili hao wanamtarajia mtoto mwezi ujao.