TANASHA7__1___1561360136_69462

Diamond Platinumz ataja siku ya harusi

Diamond platinumz amefichua siku anayo pania kumuoa mpenziiwe Tanasha.

Akizungumza na waandishi wa habari wa lebo yake ya Wasafi, katika wasafi festivals kule mjini Dar – es- salaam jana, Diamond alisema huenda siku ya harusi yake na Tanasha ni tarehe 7 Julai mwaka huu.

Diamond alitoa habari hio akijibu swali la mwanahabari mmoja aliyemuliza siku anayaopanga kumvisha pingu za maisha binti huyu wa kikenya.

Majibu yake yalikuwa ya kupendeza sana kwani alitaja kuwa atatoza watu fedha za kuingia kwenye harusi yake.

“Itakuwa sherehe ya kufana sana kwani kutakuwa na meza kumi huku 5 za kwanza zikilipiwa 200,000 ilihali zilizobaki zikilipwa shillingi 80,000 kila moja. Nathani mnafaa kuhifadhi hizo meza zote kwani kila mmoja atakumbuka tarehe 7 mwezi julai mwaka huu.”

Diamond Platnumz with Tanasha

Staa huyu wa kibao cha kanyanga na African Beauty, alisema kuwa sababu ya kupeleka harusi yake mbele kutoka tarehe 14 mwezi Februali mwaka huu ni kuwa hawakuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya hafla hio ya kiheshima ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa na mastaa wengi wa nguvu ulimwenguni.

 

Diamond Platnumz holding Tanasha
Diamond Platnumz holding Tanasha
Hata hivyo, Diamond ameamua kuwa na meza 10 pekee. Je, hilo litawezekana aje? Na Je, huenda sababu ya ndoa hii ni uja uzito wake Tanasha? sote natungoje tumwone Diamond atakalo fanya.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments