Diamond Platnumz atoboa siri ya kazi mpya, ajibu Kiba kuhusu Penseli

Screenshot_from_2019_11_02_10_30_34__1572680105_77138
Screenshot_from_2019_11_02_10_30_34__1572680105_77138
Staa na nyota wa muziki Afrika Diamond Platnumz ametangaza kazi mpya zinazokwenda kutoka hivi karibuni.

Akihojiwa katika chombo cha habari nchi jirani ya Tanzania, Diamond ametangaza kupiga kazi kubwa na Swaelee na Stefflondon.

”Nimefanya kazi nyingi za Kushikiana na wasanii, Nina collabo nyingi ndani hadi natamani nizitaje, Nina ngoma inakuja na @Swaelee, Kuna nyingine nimefanya na @Stefflondon”

Haya yanajiri muda mchache baada ya kuzushiana katika mitandao ya kijamii na Kiba.
Diamond alitamka kuwa meneja wake Boss Tale alikuwa akifanya mipango na Kiba kuhudhuria Fiesta la Wasafi.
"Usiniletee mambo ya darasa la Pili unaniiibia penseli alafu unanisaidia kutafuta .(UNIKOME)

Mwanaume huwa anaongeaga mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema..."Alichapisha Kiba.

Taarifa hizi  zilimghabisha Kiba na kuamua kutokwa na povu Insta.

Inaonekana kuwa Ali Kiba anampa Diamond onyo awache kufanya mambo anayofanya la sivyo atatoboa siri ambazo watu wengi hawafahamu.

Letu ni kukaa kitako kuona vita vya fahali hawa wawili vitafikia wapi.

Katika mahojiano Diamond Platnumz alishangaa alichomaanisha Kiba,

"Niliona post ya Alikiba, sijui alilenga nini. Ni kaka yangu, ananizidi kwa umri, namheshimu sana."