Diamond, Tanasha wanahatarisha kufungwa jela Tanzania

Screenshot_from_2019_11_17_11_31_06__1573979495_12289
Screenshot_from_2019_11_17_11_31_06__1573979495_12289
Staa na nguli wa muziki Afrika Diamond Platnumz na Tanasha Donna huenda wanahatarisha kutiwa nguvuni na mamlaka nchini Tanzania katika kipengele kipya cha kuhalalisha ndoa.

Nchi jirani ya Tanzania inasukumia kuwepo na urasmi wa ndoa kati ya raia wao.

Diamond na Tanasha ni miongoni mwa wanandoa nchini humo ambao hawajaona rasmi.

https://www.instagram.com/p/B4hsCzKAXnU/

Serikali ina mtazamo kuwa mtindo wa wanandoa kuishi chumba kimoja bila kuoana rasmi ni chanzo cha watoto wanaorandaranda mitaani.

Ndoa hizi zikivunjika, watoto hupata tabu kubwa sana na wengi huishia kuombaomba kwenye vichochoro.

Andrea TSele alitangaza kuwa wanandoa kama hao wakamatwe na kutiwa nguvuni ili wajue ubora wa kufunga ndoa.

TSele alikuwa akizungumza katika kata ndogo ya Mavanga jimbo la Ludewa Njombe .

Kinachomkera TSele ni wanaume wanaowakimbia wamama baadaye ya kuwatunga ujauzito.

" Na hawa watu wanastahili watiwe mbaroni kwa kuwa hawataki kuhalalisha ndoa ilihali wanataka kuishi kama mume na mke..." Tsele.

Tsele alihofia sana uongezeko wa watoto wanaorandaranda mitaani.
Zari The Boss Lady amenukuliwa kusema kuwa Diamond hatoi usaidizi unaotakiwa kwa watoto wao.
Hapo awali, Zari alimuonya Tanasha kuwa ajitayarishe kulea mtoto peke yake.
Inadaiwa kuwa Tanasha na Diamond wanaishi katika chumba kimoja ila hawajaona.