Tanasha Dona

Diamond,mkosi wa mafanikio! Nyimbo za Tanasha zang’aa kwenye Youtube

NA NICKSON TOSI

Wakati Diamond na baadhi ya wasanii wenzake wanapoendelea kuwa chini ya karantini kufuatia hofu ya kuwa na virusi vya Corona, mpenziwe wa zamani  Tanasha Donna anasherehekea pakubwa baada ya nyimbo zake kufanya vyema katika mtandao wa youtube mwezi huu ikilinganishwa na za Diamond.

Nyimbo za Tanasha nne alizofanya hivi karibuni zilitamalikiwa katika chati hizo baada ya wasanii wengine kutoka humu nchini kutamba katika mtandao huo.

Wimbo wa Sauti Sol Suzanna, ulitamba kwenye Youtube zikifuatia za Tanasha nyimbo nne zikiwa La Vie, Gere, Ride na Te Amo mtawalia.

tanasha

Wasanii wengine waliokuwa kwenye orodha hiyo kutokea Tanzania ni Harmonize, Rayvanny na wa humu nchini wakiwa DJ Lyta  aliyefuatwa na Diamond aliyekuwa nambari ya 6.

Baada ya ushindi huo, Tanasha aliandika hivi kwenye mitandao yake ya kijamii.

“Nyimbo bora wiki hili kwenye Youtube Kenya 2020 #1 SAUTI SOL, #2 LA VIE.. 🙏🏽🇰🇪❤️.”

“Nyimbo bora maarufu kwenye POPNABLE. #1 LA VIE.” aliandika Tanasha

tanasha

Tanasha alimshukuru Maulana kwa ufanisi wake huo, na wimbo wake wa Gere umekuwa ukifanya vyema dhidi ya Jeje wa Diamond kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni tangu waachane na msanii huyo.

“Mungu anaona kazi yako, subira makuu yapo njiani yaja! 🙏🏽🎶”aliandika Tanasha

Na kwa wale watu wanaojiita kamati ya roho chafu Tanasha alikuwa na haya.

“Tabasamu kwa wale wanaodhani hutafaulu maishani, kwa kuwa yale Mungu amekupangia hakuna mtu anaweza kuzuiya … ❤️ aliandika kidosho huyo

tanasha 1

Wakati huu ambapo ulimwengu unajaribu kupigana na virusi vya Corona, mwanamziki huyu amewataka watu kudumisha usafi kama njia ya kujikinga dhidi ya maambukizi.

 

 

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments