Diana Marua akiri kuwa hafanyi kazi. Huwa anamtegemea Bahati.

Mkewe msanii wa nyimbo za injili Bahati kupitia mtandao wa kijamii amekiri kuwa huwa hafanyi kazi bali huwa anamtegemea bahati kwa kila kitu huku akisema kuwa Bahati yuko sawa kwa kile huwa anamfanyia.

Diana Marua amekuwa aking'aa kila wakati na hata kujitia nguvu kwa kila jambo licha ya wakosoaji kumkosoa na hata kumwambia maneno makali sana.

Mmoja wa mashabiki wake walimuuliza kama anafanya kazi na alisema la.

https://www.instagram.com/p/B-lyYU1AcdY/

Shabiki huyo alizidi na kumuuliza kama huwa tu anakaa chini na kumngoja Bahati amtafutie kila kitu, bila kuogopa wala kusita alijibu kuwa hafanyi chochote.

Na mume wake Bahati hana shida yeyote kwa maana huwa anampa chochote anachotaka.

"Imagine I do not. He provides everything and he is okay with that. I do not understand why that should bother anyone. People love focussing on other people's lives." Alisema Diana.