‘Diana saidia bwana yako Bahati Kuimba.’ Willy Paul amuambia Diana Marua

  Yaonekana bifu kati ya willy Paul na Bahati imerudi tena kwani wasanii hao wameonekana kutupiana vijembe mitandaoni .

Bahati maajuzi ameandika jinsi alivyokuwa akimsaidia Willy Paul kwa kumuandikia nyimbo  na kusema ;

 “The days I used to write songs for this small boy.  I’ve missed our childish days bro #WillisRadido,”

Akijibu hilo, Willy Paul  alisema katika instagram;

“So, I’m told Bahati mtoto wa Diana said amekuwa akiniandikia nyimbo. Never. What should I tell him? Anyway, that’s me driving with my legs just to pass a little message to that boy.”

 

Posti hiyo baadaye ilifutwa. Wawili hao wamejipata mashakani  baada ya kubadilisha muziki wao kutoka 'gospel' hadi midundo ya kisasa .

Katika video nyingine iliyosambazwa mtandaoni, Pozze alidai kwamba  muziki wa Bahati ulikuwa  ukididimia. Pia alimshauri Diana Marua kumsaidia mumewe kutengeza nyimbo nzuri badala ya kutumia pesa zake.

“Bwana Diana utatuonyesha mambo kweli. Si uache hata Diana aimbe. Diana saidia Bwana yako. We unataka ulishwe Bwana anapoteza vocals we uko hapo unakula tu. Saidia Bwana.”  Alisema  Pozze

Katika posti nyingine pozze alisema

“My brother Bahati naskia ulikua uniandikia songs….. mimi? Uko sure ni mimi?? Ooh lord, give mtoto wa Diana his memory back!! He’s mistaking me for Weezdom.. Let me remind you Baba:.. Naitwa KING POZZE. Much love… Pitia home kesho kuna maji moto na ndimu atleast itakuhelp… Guys, what should i do to this small boy??”