Dili nono baada ya Sauti Sol kukutana na Obama, Savara aeleza

2ADDFE6700000578-3175385-image-m-18_1437950115984
2ADDFE6700000578-3175385-image-m-18_1437950115984
Savara wa kundi la Sauti Sol amesema kuwa sio muziki tu unafanya kundi hilo liwe pamoja ila ni madeni waliyonayo.

Katika mahojiano hapo jana katika hafla ya Oktoba Fiesta iliyoandaliwa Race Course eneo bunge la Lang'ata, muimbaji huyu amesema kuwa matatizo yanaweka kundi hili pamoja.

Soma hadithi nyingine;

"Ni shida na deni. Tumejipata katika shida na deni nyingi mpaka inabidi tukae pamoja tulipe zile deni zote...'

Aidha Savara alisema kuwa wana historia ya kuwa marafiki wakubwa kabla wapatane.

"Na pia umoja na kushirikiana na tumejuana kwa miaka 15. Tulikuwa marafiki kabla ya muziki.'

Savara amezungumzia iwapo kuna dili nono ilitoka baada ya kukutana na rais wa Marekani Barack Obama.

"Kupatana na rais wa marekani sio mchezo na inaonyesha kuwa kazi tunayofanya inafika mahali fulani. Tulikuwa na heshima sana na tukafurahi na tunashukuru wale ambao walifalicitate hiyo mambo yote..."

Katika mahojiano haya, Savara alipoulizwa swala la dili yoyote waliyopata hakuweza kueleza.

Je, huenda ikawa tukio la kihistoria la Sauti Sol kukutana na rais wa Marekani halikuzaa matunda yoyote?

Soma hadithi nyingine;

Kuhusu muziki, staa huyu amedokeza kuwa wataangusha bonge la muziki hivi karibuni na kikundi cha Ochungulo Family.

'Last week tumerekodi ngoma na Ochungulo Family inakuja."