Dili ya hela kibao, Jacque Maribe yupo mwendo wa kibiashara

Mwanahabari Jacque Maribe ni mfano na nguzo imara katika jamii tunayoishi.

Hii ni kutokana na hatua anazopiga za kibiashara.

Mrembo huyu alitoka kwenye vioo vya runinga baada ya kuhusishwa na tuhuma za mauaji.

Kwa sasa, tuhuma hizi zilizochafua jina lake hazionekani kumpiga moyo mwanadada huyu.

Kila siku anazidi kukazana na kuboresha (chapa) brand yake.

Ni dhihirisho kuwa mtu anaweza songa mbele zaidi hata baada ya kuzama katika matatizo.

Katika Insta yake, Maribe amebadilisha akaunti yake na kuonyesha ishara za kibiashara zaidi.

Iwapo mtu yeyote atataka kuwasiliana naye, basi itakuwa kirasmi sana kupitia baruameme.

Jacque Maribe ameweza kupata wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii ukilinganisha na kipindi alikuwa akifanya kazi runinga ya Citizen.

Maribe amepitia mengi pamoja na kuzuiliwa korokoroni kwa siku kadhaa kwa kukisiwa kushiriki katika mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani.

Juzi kati Maribe ameonekana katika likizo ya kula bata.

Kuna madai kuwa Maribe ni balozi wa Bountiful Safaris kando na Betty Kyalo na mcheshi Njugush.

https://www.instagram.com/p/B39pdIUHVfl/

Hii inaashiria kuwa kuna uwezekano mkubwa akawa analenga dili nono za mamilioni ukizingatia mpunga utaotoka kwa ubalozi na pia biashara za kikando zinatokana na umaarufu wake.