DJ Evolve azungumza miezi 6 baada ya kupigwa risasi na mbunge Babu Owino

Felix Orinda almaarufu kama  DJ Evolve hatimaye amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kupigwa risasi na mbunge wa Embakasi Kusini Babu Owino katika klabu moja mjini Nairobi,hatua iliyopelekea kulazwa hospitalini  kwa miezi 6.

Akiwa kwa mazungumzo na kituo cha NTV,Evolve aliambia kituo hicho kuwa tukio hilo lilimwacha akiwa amedhoofika na kutatizika kiakili.

“I have needed medication to help me sleep, I have had flashbacks from that day and it is traumatizing,”

Akiwa kwa sasa amelazwa nyumbani baada ya kuondolewa hospitalini,Orinda anasema kuwa hawezi kutumia mikono yake namna alivyokuwa akitumia kwani haiwezi kusonga kama kawaida.

“I cannot be able to move my hands past unfolding my fingers, so when I do not have them, I cannot do much as they were my tools of trade, I cannot work,”Evolve.

Wakati uo huo familia ya Evolve imesema kuwa tangu kuondolewa kwa kijana huyo kutoka hospitalini,hawajawai pata simu kutoka kwa mbunge Owino licha ya kufahamu kuwa Evolve alitoka hospitalini na yuko nyumbani.

“I saw reports on the newspapers that I had talked to Babu, those are lies because I have not spoken to anyone, this incident left me devasted and I only speak to God,” alisema mamake Orinda.

 Kwa upande wake Evolve amesema hana kinyongo chochote na Babu Owino na kuwa amewachia yote Mola.