Doktari! Karibu nyumbani, Vera ni 'wife material' usiwe na hofu. Wasema wakenya

NA NICKSON TOSI

Mwanasosholaiti Vera Sidika ni kama amepata mtu wa kumdekeza vyema raundi hii akiwa daktari kutoka Nigeria, miezi michache tu baada ya kuwachana na Jimmy Chansa kutoka Tanzania.

Amekuwa akitundika picha kwenye mitandao ya kijamii na jamaa huwa wa asili ya Nigeria kwa jina Tommy Daniel , nyingi ya picha hizo akiwa anazitundika kwenye Instagram na kumuita majina ya kumsifia kama cute.

Tommy ni mwanagainagolojia na mwanamitindo wa zamani aliyekuwa anafanyia kazi hiyo Dubai.

Tommy alituma ujumbe huu kwenye Instagram yake, ujumbe uliokuwa unamwelekea Vera.

 Kuwa salama huko uliko, aliandika Tommy
 Vera kwa upande wake alijibu kwa madaha akaandika hivi.
Asanti hun🥰❤️😘.

Baada ya wakenya kuona jumbe hizo walikuwa na haya ya kuandika katika mitandao mbailmbali.

gw374580 @queenveebosset soo mliachana na bwanako wa tanzania?

shishythemodel Wueeehh ninani anayeona hiihahah @timmytdat ujaluo shuma ni doshi🤣🤣😆😆

 catekaddy @queenveebosset doctari mwingine?no, jaribu a shamba boy Vee.