Domo kaya! Mahakama yamtaka Ole Kina kufika mbele yake kuhusiana na matamshi ya Uchochezi

Mahakama ya Nairobi imemtaka seneta wa Narok Ledama Ole Kina kufika mbele yake mnamo Juni 2 kujibu madai ya uchochezi na matamshi ya kuibua hisia mseto miongoni mwa wakaazi.

Kulingana na makosa yanayomkabili Ole Kina, inadaiwa kuwa Februari akiwa katika kipindi kwenye televisheni ya humu nchini, alizungumza maneno ambayo yangeweza kuwachochea wakaazi wa eneo fulani na kusababbisha mapigano ya kijamii.

The prosecutor accuses the senator of uttering: “Maasai issues will be articulated by Maasais not Manje who is … who…who can be able to get an audience in Mount Kenya,” matamshi ambayo yanadaiwa kuwa huenda yangeibua hisia mseto miongoni mwa jamii ya Maasai nchini.

Hakimu wa mahakama ya Nairobi Kennedy Cheruiyot ametoa notisi hiyo baada ya mlalanmishi James Gachoka kuelezea mahakama kuwa serikali ilikuwa imesita kumshtaki kiongozi huyo.