Domo Moto ! Tazama jinsi Gavana Mike Sonko alivyowakomesha vikali Mwaura na Millie Odhiambo.

Ujumbe wa Sonko katika facebook
Ujumbe wa Sonko katika facebook
Gavana wa Nairobi Mike Sonko   anafahamika kama mtu asiyeweza kuthibitiwa na hasa kuhusu yanayotoka kinywani mwake .Sonko amepata sifa nyingine  mpya za kutoweza kubana siri baada ya kuamua kupasua mbarika wakati wa hafla ya misa ya wafu ya aliyekuwa  mbunge wa Kibra Ken Okoth aliposema kwamba alifahamu Okoth alikuwa na mpenzi wa pembeeni mwakilishi wa kaunti  Anne Thumbi na  walizaa naye mtoto . Sonko aliamua kuwajibu kwa bonge la posti kwenye facebook ambalo  limezagaa mitandaoni na watu wanaendelea hata kusalia vinywa wazi . Tazama

Hatua ya Sonko kuyasema hayo hadharani haikuwafurahisha wengi na miongoni mwa walioamua kumsuta Sonko kwa hatua hiyo yake ni Seneta mteule Isaac Mwaura na Mbunge wa Suba North Millie Odhiambo . Lakini Sonko ni nani? Amewajibu kwa ujumbe mkali kwenye facebook na mitandao mingine ya kijamii na akaongeza kwamba atazidi kuwafichua wanasiasa wanaozaa watoto nje ya ndoa na kisha kukwepa majukumu yao .