Don't bleach! Zari atoa ushauri kwa wanadada dhidi ya kubadili ngozi zao

101964452_260926751788207_7323067816041202705_n
101964452_260926751788207_7323067816041202705_n
Mwanasosholaiti wa Uganda na mama wa watoto watano Zari Hassan amekuwa akisemwa zaidi kuhusiana na jinsi anavyoishi maisha yake  ya kifahari.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Zari ametundika picha zake za awali akiwasihi wanawake kutobadili ngozi ya mwili wao ama bleaching kama njia ya kuwavutia watu.

Katika picha hizo zote mzaliwa huyu wa Afrika Kusini alikuwa kati ya miaka 17-18  wakati ambapo alikuwa ameanza kuibukia katika sanaa tofauti.