Double Tragedy! Jamaa awapachika mimba dada wawili wa toka nitoke

sad man
sad man
Justus* hakujua kwamba kaburi analojichimbia litamfikisha pabaya au kugeuka kuwa kisa cha  kumpa matatizo sio haba. Alianza  uhusiano  na  mtu na dadake na katika chezo chezo za ujana akashiriki mapenzi na wote.

Kama  filamu na kwa bahati  mbaya, wote wakapata ujauzito na sasa kinachoendelea  ni kutafuta  suluhisho na jinsi ya kujinasua kutoka mtego aliojipata. Je, yote yalianzia wapi? Na Vipi? Masaibu yake yalianza wakati alipomtongoza Veronica kutumia dadake ambaye alikuwa akipeleka jumbe  zake kwa dadake mkubwa. Wakati wote pakitokea jambo kwa sababu ya hofu ya kuonekana, Justus alikuwa akimtumia  Valarie kufikisha ujumbe wake kwa Veronica. Bila kujua, Valerie naye pia alikuwa anamtaka  na bila kujua mipaka ya damu, alianza naye kuzibana zile jumbe na kisha kuwasilisha majibu yasiotarajiwa  kwa Justus. Ikafika wakati hata dada hao wawili wakawa hawapatani kwa ajili ya mgongano wa mawasiliano kati  yao na Justus .

Alipotoka Eldoret kwenda Nakuru chuo kikuu, Veronica alijua kwamba yeye na Justus walikuwa katika uhusiano wa kudumu na hata kufanya mipango yao ya siku za baadaye. Kule Eldoret,Valerie alipata fursa sasa ya kuweza kumsogea kwa karibu mpenzi wa dadake. Mwanzoni,  Justus alijifanya kuwa mstaarabu akikataa juhudi za ‘shemeji’ yake kumtia katika majaribu lakini muda usiokuwa mrefu, wawili hao walianza ficha ficha za usiku na hatimaye kujipata wameshiriki mapenzi.

Kilichodhaniwa kitakuwa cha kwanza na cha mwisho, kiligeuka kuwa mazoea ya mara kwa mara na kabla hajajua  hatari  iliyomgonja, Justus alikuwa akilala na dada wote wawili. Wakati mmoja wa likizo akiwa nyumbani, Veronica alianza kugundua kwamba dadake naye pia alikuwa akimpenda Justus kwani wakizungumza kumhusu, alimwangalia machoni na hata akaanza kumshawishi kwamba yeye Veronica hakufaa kuwa mpenzi wa  Justus kwa sababu wametofautiana kwa vitu vingi. Veronica alianza kugundua kwamba dadake alifahamu vitu vingi vya kibinafsi kumhusu mpenzi wake Justus na hilo lilimpa sana hofu.

Alipomuuliza Justus, usaliti wake ulikuwa bayana kwani tapatapa zake za kujitetea na kujishuku zilimfanya apasue mbarika akisema yote yaliyokuwa yakifanyika kati yake na dada hao wawili. Veronica alikatiza uhusiano wake papo hapo na  Justus na kurejea Nakuru. Valerie kwa pande wake aliposikia kilichotokea, alifurahi sana akiiona ile kama fursa yake sasa kuwa mpenzi wa pekee wa Justus.  Mwezi huo septemba 2018, Veronica alikosa kuona siku zake za hedhi, Bila kujua, dadake kule Eldoret pia alikuwa keshapimwa ujauzito na kugunduliwa kwamba alikuwa na mimba. Aliyekuwa wa kwanza kumueleza Justus kwamba ana mimba ni Veronica aliyempigia  simu kumpa habari hizo na akitaka kujua kinachofaa kufanyika.Uhusiano wao ulikuwa umekwisha kwa sababu ya usaliti wake lakini sasa mimba ilikuwa imesbabisha mvurufo zaidi wa kiakili kati yao. Vero hakuwa tayari kutoa mimba .

Wiki hiyo, Justus hakujitayarisha kwa uzito wa habari zilizomngoja kwani wikendi walipokutana na Valarie, naye alimpa bonge  la habari kwamba alikuwa anatarajiwa mtoto wake. Akifikiria dada hao walikuwa wakimfanyia  utani, Justus alifichua kwa Valerie kwamba Vero naye pia alikuwa na mimba yake –Hapo ndipo Justus alipotamani ardhi ipasuke na immeze mzimamzima .