Serikali ya kaunti ya Kajiado imewasimamisha kazi wafanyikazi wake wawili baada ya mwanamke mmoja kuaga dunia kwa kujirusha kutoka ambulansi wakati mtoto wake alipofariki . Mwanamke huyo aliyetambuliwa kama Naiso Leslie aliichukua hatua hiyo wakati mtoto, Solomon Lesie, alipoaga dunia akikimbizwa kwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Kajiado . Miili yao imepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali hiyo ilhali ambulansi iliyohusika katika tukio lenywewe imekokotwa hadi katika kituo cha polisi cha Kajiado .
Waziri wa afya wa kaunti Esther Somoire amethibitisha kwamba dereva na muuguzi waliokuwa katika zamu wakati w atkio hilo ndio waliosimamishwa kazi . OCPD wa Kajiado central Daudi Loronyokwe amesema wawili hao tayari wameandikisha taarifa na polisi huku uchunguzi kuhusu kisa hicho ukiendelea .
Mvulana aliyeaga dunia alikuwa amelazwakatika kituo cha cha afya cha Bisl kabla ya kupendekezwa ahamishwe katika hospitali ya rufaa ya kajiado .Kulingana na OCPD ,mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 26 aliufungua mlango wa nyuma wa ambulansi na kuruka nje wakati gari hilo likiwa katika mwendo wa kasi .