Katika Memo ya tarehe 10 mwezi Mei Haji amesema malipo hayo yalitolewa kwa Nyali Capital Ltd (NCL). Amesema uchunguzi umefichua kwamba Nyoike aliitumia afisi yake kufanikisha kuwekwa kwa NLC katika orodha ya kampuni za kulipwa pesa hizo kwa huduma na bidha ziliztolewa kwa KPA.
Haji pia amesema ushahidi umoenysha kwamba hapakuwa na mkataba wowote kati ya KPA na Nyali Capital Limited isopokuwa barua zilziotiwa saini na mamenaja wa KPA kwamba KPA Ingetoa malipo ya kuipa NLC fedha kutoka kwa kampuni zilizokuwa zikifadhiliwa na kampuni hiyo .
Kwa sababu ya hilo Haji amependekeza kushtakiwa kwa Nyoike ,mkewe Jacinta Wambugu, kakake Alfred Hinga, Isaac Obunga (karani wa KPA), Peter Kinyanjui (mkurugenzi wa NCL) na Nyali Capital Limited. Mwezi uliopita aliyekuwa Mkuu wa KPA Daniel Manduku aliondolewa mashtaka ya ufisadi baada ya Haji kuktaa kuidhinisha mashtaka dhidi yake .
Alikuwa ameshtumiwa kw a kutoa tenda ya ujenzi wa ghala la uhifadhi wa mizigo katika Nairobi Inland Container Depot (ICD) kwa njia isiofaa.Manduku alijizulu mwezi uliopita .