Drama za Ng'ang'a zashika kasi Marekani, Snoop Dogg atupa dongo (+Video)

Snoop-Dogg
Snoop-Dogg
Sakata na Drama za muhubiri tata James Ng'anga zilizogonga vichwa vya habari wiki iliyopita sasa zimefika anga za Marekani.

Rapa na staa mkubwa Snoop Dogg amechapisha video ya Ng'an'ga katika mtandao wake maridhawa wa Insta.

Haya yanajiri muda mchache baada ya muhubiri huyu kusema kuwa wanasambaza video zake ni Ibilisi wanaotaka kumshusha.

Soma hadithi nyingine:

Ng'ang'a anahoji kuwa video zile ni za maadui wanaolenga kumshusha na kumchafulia jina.

“Huwa nafanya mambo mengi mazuri. Nawapa watu chakula, lakini hao wanakata tu (video)  ile nimeongea vibaya kwa sababu ni watu wana mapepo.” Alisema Ng’ang’a

Ng’ang’a alikana taarifa za kutamani kujiua.

“Niliskia taarifa kuwa kuna watu wanasema kwamba waliniona nikiendesha V8 nikiwa na mawazo, ni kama nataka kujia.”

Snoop Dogg alichapisha video hiyo na akafuatisha caption ya kejeli.

https://www.instagram.com/p/B2unpZynq7F/

Kulingana na rapa huyu, hivi ndivyo kasisi anavyopaswa kumwadhibu mtu sadaka inapokosa kutoshea.

Asichoelewa Snoop Dogg ni kuwa tendo la kuwazaba kofi waumini ni njia moja ya kufanya ibada.

Soma hadithi nyingine:

James Ng'ang'a amewaomba watu wakome kueneza habari feki,

Hebu tuwe wakweli. Mbona nijiue? Angalia bibi wangu mrembo. Nitamwachia nani nikijiua.” alijitetea Ng’ang’a

“Nitaachia nani magari yangu na jumba langu. Labda niwafahamishe majirani zangu ni wazungu. We just say ‘hi’ to each other, hakuna mambo ya kushinda tukibishania mlango..” Aliendelea kujinadi

Aliwaonya mahasidi wake wakome kueneza taarifa za uongo kuhusu ibada zake.