Drogba aitakia ushindi Ivory Coast ikikabana koo na Mali

Ivory Coast almaarufu kama 'The Elephants' itaingia dimbani hii leo kukabana koo dhidi ya Mali kusaka tiketi ya kutinga katika  robo fainali ya kombe la AFCON saa moja usiku. Drogba,aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho cha Elephants ameonyesha ushabiki wake kwa timu yao ya taifa kwa kuwatakia kila la heri kwenye mchuano huu wa leo.

Ivory coast na Mali zimo katika nafasi moja kwa orodha  ya fifa zikishikilia nafasi ya 62. Mali ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi E baada ya kutoka sare moja na kupata ushindi Mara Mbili.

Ivory coast ambao ni mabingwa mara mbili wa taji hilo walimaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi D baada ya kushinda mechi mbili na kupoteza moja. Huenda Ivory coast ikazikosa huduma za beki wa Totenham Hotspurs ya Uingereza,Serge Aurier aliyepata jeraha kwenye mechi ya mwisho ya makundi. Kwa upande wao Mali, kila mchezaji yupo fiti kukigaragaza hii leo.

Kwingineko ni kuwa Tunisia itashuka dimbai kukipiga dhidi ya Ghana saa nne usiku.