Drogba awasilisha nyaraka zake za kuwania urais wa shirikisho la soka Ivory Coast

Maelfu ya watu wajikusanya nje ya afisi za Soka katika taifa Ivory Coast pale mchezaji wa zamani wa timu ya taifa Didier Drogba alipokuwa anawazilisha karatasi zake za kuwania nafasi ya urais wa shirikisho la soka la taifa hilo la Afrika ya mashariki.

Drogba wa miaka 42 ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika ni miongoni mwa wawaniaji wanne ambao wanataka kuwa vinara wa shirikisho wa taifa hilo .

Kando na kupata uungwaji mkono wa vilabu vitatu kati ya vilabu 14 vinavyoshirikis ligi kuu ya taifa hilo ,ni sharti mchezaji huyo wa zamani apate uungwaji mkono wa vilabu viwili vinavyoshiriki katika liguu ya daraja ya pili na pia kuungwa mkono na watu  watano kutoka vitengo tofauti vikiwemo Makocha,Madaktari ,uongozi wa sasa wa shirikisho hilo na wachezaji wenza wa zamani wa taifa hilo pamoja na waamuzi .

Drogba aliewasilisha karatasi zake mida ya saa 5 jioni na kupokelewa na mashabiki wake waliokuwa wanamngoja nje ya afisi kuu za shirikisho la michezo katika taifa hilo.