Duale atimuliwa huku nafasi yake ikichukuliwa na Amos Kimunya

Aden-Duale
Aden-Duale
Mbunge wa Kipipiri Amos Kimunya ameteuliwa kuchukua nafasi ya Aden Duale kama kiongozi wa wengi kwenye bunge la Kitaifa.

Mabadiliko hayo yamefanyaka baada ya kuandaliwa kwa kikao kikuu cha wabunge wa chama cha Jubilee hii leo na kilichohudhuriwa na rais Kenyatta pamoja na naibuye William Ruto.

Wakati uo huo mbunge Aden Keynan ameteuliwa kama msajili wa muungano wa Jubilee.

Mabadiliko hayo yanajiri saa chache tu baada ya wabunge 126 kati ya 179 kupiga kura ya kutokuwa na imani na Duale katika utendakazi wake.