crime

Dunia imepasuka: Ajuza wa miaka 97 abakwa Bungoma

Ajuza mwenye wa miaka 97 anapokea matibabu katika hospitali moja mjini Bungoma baada ya kudaiwa kubakwa na mtu asiyejulikana usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Kimukung’i katika eneo bunge la Kanduyi kaunti ya Bungoma.

Ajuza huyo amesema kijana ambaye hamfahamu alifungua mlango wa nyumba yake na kuanza kumtendea unyama huo kabla yake kupiga nduru iliyomfanya atoroke.

Majirani waliokimbia kumuokoa wamesema mshukiwa alitoka kwenye nyumba hiyo akiwa nusu uchi na kukimbia bila kutambuliwa.

Kwingineko, mzazi mmoja wa mwanafunzi aliyefanya mtihani uliopita wa darasa la nane akiwa amejifungua wiki moja kabla ya mtihani katika shule ya msingi ya Botwa eneo bunge la cherangany kaunti ya Trans Nzoia na kupata alama ya mia mbili hamsini na nne anataka mwanamume
aliyempachika mwanawe mimba kutiwa mbaroni.

Peter mayende ambaye ndiye babake mtoto huyo wa miaka kumi na sita anasema mwanawe alipachikwa mimba na bwana mmoja mhudumu wa bodaboda mwezi wa pili na alikaa nyumbani muda huo wote bila kuhudhuria masomo.

Ametaka serikali imchukulie hatua mwanamume huyo ambaye inadaiwa amekuwa na tabia hizo za kuwapachika watoto wengine kumi mimba eneo hilo na Kuendelea kuwa huru.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments