Dunia Isimame Nishuke: Baba Auawawa Baada Ya Kubaka Maiti Ya Mwanawe (AUDIO)

death
death
Mwanaume mmoja wa miaka arobaini na tano aliaga baada ya kupigwa na jamaa na marafiki, kufuatia kitendo cha 'kubaka' mwili wa mwanawe wa miaka kumi na nne aliyeaga siku moja iliyopita katika kijiji cha Kiwanja Ndege, eneo la Mau Sammit.

Kulingana na majirani, mwanafunzi huyo wa darasa la sita aliaga baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Aidha, famlia na waombolezaji walijawa na ghadhabu baada ya kumfumania mwanaume huyo kwa jina Hassan, akifanya mapenzi na mwili wa mwanawe, suala lililowasababisha kumpiga hadi kumuua.

Kulingana na chifu wa eneo hilo, Joseph Ng'eno unywaji wa pombe haramu ulichangia pakubwa kitendo cha mwanaume huyo, huku akitoa wito kwa familia zote kuwa waangalifu katika masuala yanayowahusu watoto.

Kitendo hicho kiliwaacha wakazi wa eneo hilo vinywa wazi huku familia hiyo wakilazimika kufanya tambiko kulingana na mila na tamaduni zao ili kuzuia maafa yanayoweza kusababishwa na kitendo hicho.

&feature=youtu.be