EACC kuwajulisha washukiwa kabla ya kuchunguza akaunti zao za benki

Siku ya Jumatano jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufaa liliamua kwamba tume ya EACC inapaswa kuwajulisha washukiwa kabla ya kutafuta agizo la mahakama kuruhusiwa kuchunguza akaunti zao za benki.
 Mahakama ilisema kuwa agizo la mahakama linaweza kutolewa tu iwapo mshukiwa amekataa kutoa taarifa kwa hiari.

Uamuzi huu ulitolewa baada ya tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC kupata kibali kutoka kwa mahakimu wa mahakama ya Kibera mwaka 2015 kuzichunguza akaunti za wakili Tom Ojienda kuhusiana na kupokea kwake kwa shilingi milioni 280 kutoka kwa kampuni ya sukari ya Mumias.

 Uamuzi huu huenda ukawa hatiri kwani ina maana kuwa ni lazima washukiwa wajulishwe kuwa wanachunguzwa na iwapo utakubalika utawaathiri polisi pamoja na mashirika ya usalama.

.