EACC: ufisadi na ukosefu wa ajira ni changamoto kwa wakenya

Kuongezeka kwa kesi za rushwa na ukosefu wa ajira kwa vijana bado imebaki kuwa wasiwasi mkubwa miongoni mwa wakenya.

Katika uchunguzi uliotolewa na EACC  kuhusiana na rushwa, asilimia 49.4 ya wakenya walisema ufisadi bado ni changamoto kubwa kwao.

Hii ni licha ya Rais Uhuru Kenyatta kujaribu kupambana na ufisadi nchini.

Utafiti huo ulifanywa kati ya Novemba 16 na Disemba 19, mwaka 2018.

Mahojiano yalifanywa katika kaya 5,942 zilizopigwa sampuli kutoka kaunti 47.

Ripoti hiyo ilionyesha kuwa ukosefu wa ajira bado ni hoja kuu huku asilimia 36.8 wakisema kuwa bado ni changamoto kubwa.

Umasikini na njaa ni ya tatu katika orodha hiyo na asilimia 27.2 ikifuatiwa na gharama kubwa ya maisha ikiwa na asilimia 16.

 Asilimia 13.40 ya wakenya wanasema kuwa miundombinu ni changamoto huku asilimia 11 wakisema kuwa hali mbaya ya uchumi ndio changamoto yao kubwa ikilinganishwa na asilimia 10.20 ambao walizua wasiwasi juu ya ukosefu wa usalama.

Katika mapendekezo yake, shirika la ujasusi lilisema kwamba kunahitajika uchunguzi wa wahalifu wafisadi kama hatua muhimu ya kupunguza kuongezeka kwa ufisadi.

Kulingana na ripoti hiyo, asilimia 27.7 ya wakenya wanafikiria uchunguzi ni muhimu katika hatua za kuzuia uovu huo.

Asilimia 13.2 walisema kuwa elimu ya umma ni muhimu, huku asilimia 11.7 wanahisi kuwa mashtaka itakuwa njia bora ya kumaliza ufisadi.

Asilimia 7.7 ya wakenya wanahisi kwamba uwepo wa ajira ni muhimu sana katika kudhibiti ufisadi ikilinganishwa na asilimia 7.2 ambao walisema uwepo wa  sheria kali itasaidia kumaliza changamoto hiyo.

Asilimia 4.9 walisema kuwa mabadiliko ya mitazamo ni chaguo bora katika mapigano ya ufisadi.

EACC ilipendekeza uhakiki na uchambuzi wa miundo, mifumo, na michakato ya serikali ya kitaifa na kaunti ya usimamizi na uwajibikaji.

Ripoti hiyo ilipendekeza zaidi uhakiki na uimarishaji wa sheria za kupambana na ufisadi na maadili, maendeleo na utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa ushiriki wa raia na ushiriki katika kufanya maamuzi, na uimarishaji wa mahakama kuondoa udhaifu wa kimfumo, unyanyasaji, na ufisadi.

Kutoka kwa uchunguzi huo, asilima 35 ya wakenya wangelipa hongo ili kupata huduma ya haraka.