Kupitia barua kwa mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya ,afisa mkuu mtendaji wa Eacc Twalib Mbarak amesema kwamba uamuzi huo haufai na ni ukiukaji wa sharia na vipengee kadhaa vya katiba .
Katika barua yake Mbarak ameonya kwamba afisa yeyote wa kaunti anayetekeleza maagizo hayo kutoka kwa baraza la magavana atawajibikia binafsi hatua hiyo ikiwemo kushtakiwa . Mbarak amemuonya Oparanya kwamba barua yake ilikuwa ikitoa maagizo yanayokiuka sharia na kwamba wote katika serikali za kaunti watakaotekeleza maagzo hayo wanajitioa katika hatari ya kuchukuliwa hatua za kisheria .
Baraza la vyombo vya habari , muungano wa wamiliki wa vyombo vya habari na chama cha wahariri vyote vilikuwa vimekashifu hatua hiyo ya baraza la magavana dhidi ya kampni ya NMG.
Wamiliki wa vyombo vya habari jumatano walikuwa wametoa taarifa kulaani uamuzi huo wa magavana na kusema kwamba hatua ilizochukua ina hatari ya kuvuruga uhusiano kati ya taasisi za umma na vyombo vya habari kado na kuweka mfano mbaya . Muungano huo ulisema COG kama taasisi yoyote ya umma au mtu binafsi ina haki ya kulalamika kuhusu habari zinazochapishwa kuihusu lakini kwa njia ifaayo . Taarifa iliyoleta utata ilihusu magavana wanane ambao Eacc inawachunguza kwa tuhuma za ufisadi .