Eden Hazard kukosa mechi ya kwanza ya msimu

GettyImages.1149894170
GettyImages.1149894170
Eden Hazard anatarajiwa kukosa mchuano wa kwanza wa Real Madrid wa La liga baada ya kupata jeraha akiwa mazoezini. Hazard alijiunga na Real Madrid kwa kima cha millioni mia moja na sasa anatarajiwa kukosa mechi dhidi ya Celta Vigo na Real Madrid inayoterajiwa kugaragazwa siku ya Jumapili.

Hazard alishiriki mechi sita za kujiandaa kwa msimu huku akicheka na wavu mara moja kwenye mechi hizo. Kando na Hazard, mlinzi wa Kulia, Dani Carvajal pamoja na Winga wa kushoto Marco Asensio pia wanatarajiwa kutokuwepo kwani Carvajal anahudumia marufuku ya kandi nyekundu ya msimu uliopita huku naye Asensio akiuguza jeraha la kiuno.

Kakake Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesema kuwa klabu ya Real Madrid bado inauwezo wa kukamilisha uhamisho wa kiungo huo mwaka huu.

Pogba amehusishwa na uhamisho kwenda ugani Santiago Bernabue kwa muda sasa na huenda akijiunga na Madrid iwapo Neymar hatakamilisha uhamisho wake kwenda uhispania.