EFL: Furaha kwa wanabunduki baada ya kupata ushindi wa 5-0

Arsenal.000
Arsenal.000
Kieran Tierney aliichezea Arsenal kwa mara ya kwanza na mshambulizi kinda Gabriel Martinelli akafunga mabao mawili Gunners walipowanyanyua Nottingham Forest mabao 5-0 katika raundi ya tatu ya kombe la Carabao.

Martinelli alianza kufunga katika kipindi cha kwanza, huku Rob Holding akifunga la pili baada ya mapumziko kabla ya mabao ya dakika za mwisho ya Joe Willock na Reiss Nelson.

Martinelli kisha akaongeza bao la pili. Wakati huo huo Manchester City walifuzu kwa raundi ya nne ya kombe hilo kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Preston.

Kwingineko, Danny Welbeck alifunga bao lake la kwanza katika kipindi cha karibia mwaka mmoja Watford walipowanyuka Swansea na kufuzu kwa raundi ya nne ya kombe la Carabao. Watford, ambao walicharazwa mabao 8-0 na Manchester City katika ligi ya Primia jumamosi, walianza kufunga kwa bao la kichwa cha Welbeck.

Mshambulizi huyo wa Uingereza aliyejiunga na Watford kutoka Arsenal kwa uhamisho huru mwezi Agosti, alikua hajafunga bao lolote katika siku 334. Alipata jeraha la mguu Novemba ambalo lilimweka nje kwa miezi sita.

Hayo yakizijiri, Lionel Messi alipata jeraha katika mechi yake ya kwanza msimu huu, Barcelona walipopata ushindi dhidi ya Villarreal ugani Nou Camp. Messi, ambaye alikua amepona jeraha la mguu kabla ya mechi hiyo, aliondolewa kunako kipindi cha pili baada ya kupata matatizo ya paja.

Raia huyo wa Argentina, aliyekuwa akianza kwa mara ya 400 kwenye La Liga, alitoa kona na kumpelekea Antoine Griezmann kufunga bao. Barcelona ilipanda nafasi nne kwenye jedwali la La Liga.

Humu nchini, Kenya inasubiri zaidi hii leo kwa ushindi katika michuano ya kombe la dunia la voliboli la FIVB, baada ya kupoteza kwa Uchina jana huko Japan. Malkia Strikers walipoteza katika mechi yao ya nane kwenye kipute hicho. Licha ya kupoteza huko, walionyesha mchezo mzuri hasa kutoka kwa kinda Sharon Chepchumba. Leonida Kasaya na Mercy Moim walimaliza na alama saba kima mmoja.